Majina ya Walioitwa Kazini TRA 2026

July 12, 2026

 Majina ya Walioitwa Kazini TRA 2026

TRA Yatoa Taarifa Muhimu Kuhusu Nafasi Mpya za Ajira kwa Walio kwenye Candidate Database

Dar es Salaam, Julai 12, 2026 – Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewakumbusha waombaji wa ajira kuwa zoezi la ajira lililofanyika kati ya Februari na Juni 2025 lilihusisha kujaza nafasi 1,596 katika idara mbalimbali za mamlaka hiyo.

Baada ya mchakato huo kukamilika, waombaji waliofanikiwa walipewa ajira, huku wengine waliokidhi vigezo lakini hawakupata nafasi wakiwekwa kwenye TRA Candidate Database ili waweze kuzingatiwa pindi nafasi nyingine zitakapopatikana.

TRA imeeleza kuwa nafasi mpya za kazi zitakazojitokeza kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo kustaafu kwa watumishi au kuondoka kazini, zitajazwa kwa kutumia orodha hiyo ya waombaji waliopo kwenye Candidate Database.

Kwa sababu hiyo, waombaji wote waliopo kwenye hifadhidata hiyo wanashauriwa kufuatilia mara kwa mara barua pepe (email) walizotumia wakati wa kutuma maombi ya kazi. Pia wanapaswa kutembelea tovuti rasmi ya TRA pamoja na kurasa zake rasmi kwenye mitandao ya kijamii ili kupata taarifa za ajira na mawasiliano mengine muhimu yanayotolewa na mamlaka hiyo.

TRA inasisitiza kuwa taarifa zote rasmi kuhusu mchakato wa ajira zitatolewa kupitia njia zake za mawasiliano zilizoidhinishwa, hivyo waombaji wanapaswa kuwa makini na kuepuka taarifa zisizo rasmi kutoka vyanzo visivyoaminika.