HESLB Yafungua Dirisha la Maombi ya Mikopo 2026/2027
HESLB Yafungua Dirisha la Maombi ya Mikopo 2026/2027
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Dr. Bill Kiwia leo Juni 19, 2026 amefungua rasmi dirisha la maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2026/2027, huku mchakato wa uombaji mikopo ukitarajiwa kuhitimishwa Agosti 31, 2026.
Miongozo iliyozinduliwa ni pamoja na ule wa utoaji mikopo kwa wanafunzi wa Shahada za Awali, Stashahada, Stashahada ya Juu ya Mafunzo ya Sheria kwa Vitendo (Postgraduate Diploma in Legal Practice) pamoja na Mwongozo wa Ruzuku za Samia Scholarship.
Dirisha la maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2026/2027 litakuwa wazi kwa siku sabini na tatu (73) kuanzia leo na litafungwa rasmi Agosti 31, 2026.