Ajira Wizara ya Afya 2026 Nafasi 63 za Madaktari na Wauguzi (Medical Officer II & Assistant Nursing Officer II)
Ajira Wizara ya Afya 2026 Nafasi 63 za Madaktari na Wauguzi (Medical Officer II & Assistant Nursing Officer II)
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Wizara ya Afya Tanzania imetangaza nafasi mpya za kazi kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 63 za mkataba wa mwaka mmoja (1).
Nafasi hizi zinahusisha kada za afya ambapo zimetangazwa nafasi za Daktari Daraja II (Medical Officer II) pamoja na Afisa Muuguzi Daraja la II (Assistant Nursing Officer II).
Muhtasari wa Ajira Wizara ya Afya 2026
- Mwajiri: Wizara ya Afya
- Mamlaka iliyotangaza: Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
- Aina ya ajira: Mkataba wa mwaka mmoja (1)
- Idadi ya nafasi: 63
- Mwisho wa kutuma maombi: 18 Julai 2026
1. Daktari Daraja II (Medical Officer II) – Nafasi 23
Majukumu ya Daktari Daraja II
Mteule wa nafasi hii atafanya majukumu yafuatayo:
- Kutoa huduma za matibabu hospitalini zinazohusiana na magonjwa mbalimbali.
- Kuhudumia wagonjwa wa watoto, akina mama pamoja na kufanya upasuaji wa kawaida na dharura.
- Kutoa na kusimamia elimu ya afya kwa jamii.
- Kutunza na kutumia takwimu za afya kupitia mifumo husika.
- Kuchunguza, kufuatilia na kuzuia milipuko ya magonjwa.
- Kuandaa elimu ya kujiendeleza kwa watumishi wa afya.
- Kusimamia na kuelekeza watumishi walio chini yake.
- Kubuni na kuendesha tafiti pamoja na kusambaza matokeo.
- Kuandaa mikakati ya kuongeza ubora wa huduma za afya.
- Kuandaa mipango na makisio ya bajeti ya huduma za afya.
- Kushiriki katika ukaguzi wa huduma za tiba (Medical audit) na maboresho ya ubora wa huduma.
- Kufanya majukumu mengine atakayopewa na mkuu wa kazi.
Sifa za Mwombaji – Medical Officer II
Mwombaji anatakiwa kuwa na:
- Shahada ya Udaktari kutoka chuo kikuu kinachotambuliwa na Serikali.
- Awe amesajiliwa na Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).
Ngazi ya Mshahara
- TGHS E
2. Afisa Muuguzi Daraja la II (Assistant Nursing Officer II) – Nafasi 40
Majukumu ya Afisa Muuguzi Daraja la II
Mteule atakuwa na majukumu yafuatayo:
- Kutoa huduma za uuguzi.
- Kukusanya takwimu muhimu za afya.
- Kuwaelekeza kazi wauguzi walio chini yake.
- Kuelimisha wagonjwa na jamii kuhusu matatizo ya kiafya.
- Kutoa huduma za kinga na uzazi.
- Kufanya majukumu mengine atakayopewa na mkuu wa kazi.
Sifa za Mwombaji – Assistant Nursing Officer II
Mwombaji anatakiwa kuwa na:
- Stashahada (Diploma) ya Uuguzi kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
- Awe amesajiliwa na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania.
Ngazi ya Mshahara
- TGHS B (MOH)
Masharti ya Jumla ya Waombaji
Waombaji wote wanapaswa kuzingatia masharti yafuatayo:
- Awe raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
- Asiwe na umri zaidi ya miaka 45.
- Ambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
- Ambatishe vyeti vya taaluma na vyeti vya kitaaluma kutoka bodi husika.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vimehakikiwa na mamlaka husika kama TCU, NECTA au NACTVET.
- Waombaji wenye taarifa za kughushi watachukuliwa hatua za kisheria.
- Waajiriwa wa Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba bila kufuata taratibu husika.
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba bila kibali maalum.
Jinsi ya Kuomba Ajira Wizara ya Afya 2026
Maombi yote yanatakiwa kutumwa kwa njia ya kielektroniki kupitia Recruitment Portal ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
Waombaji wanapaswa kuhakikisha wanaambatanisha:
- Barua ya maombi ya kazi iliyosainiwa.
- Vyeti vya elimu.
- Vyeti vya kitaaluma.
- Cheti cha kuzaliwa.
- Nyaraka nyingine zinazohitajika kulingana na nafasi husika.
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 18 Julai 2026.