Nafasi za Kazi za Muda Rombo District Council

June 12, 2026

Nafasi za Kazi za Muda Rombo District Council

Nafasi za Kazi za Muda Rombo District Council

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo anatangaza nafasi mia moja (100) za ajira ya muda ya kukusanya Ushuru/Mapato katika Halmashauri ya Wilaya ya Rombo.

SIFA ZA MWOMBAJI

 * Awe amehitimu Elimu ya kidato cha nne/sita.

 * Awe na Elimu ya kuanzia Stashahada (Diploma) na kuendelea kwenye fani ya Biashara/ Uhasibu.

 * Awe tayari kufanya kazi sehemu yoyote atakayopangiwa na Halmashauri.

 * Awe mkazi wa Rombo.

MAJUKUMU YA KAZI

 * Kukusanya mapato

 * Kubaini vyanzo vya mapato

 * Kuwa kwenye kituo chake cha kazi wakati wote.

MASHARTI YA JUMLA

i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri kati ya miaka 18 hadi miaka 40.

ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.

iii. Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina yao.

iv. Maombi yote yaambatane na cheti cha kidato cha nne, sita na vya taaluma.

v. Awe na kitambulisho cha mpiga kura, Kitambulisho cha Taifa au namba ya kitambulisho.

vi. Picha mbili "Passport size" ya hivi karibuni iandikwe jina nyuma.

vii. Waombaji wenye ujuzi wa kutumia computer na wenye fani ya udereva na wenye pikipiki binafsi watapewa kipaumbele zaidi.

viii. Awe anaweza kutumia simu janja (Smart Phone).

ix. Awe na Wadhamini wawili (02)

x. Maombi yote yawasilishwe masijala ya Mkurugenzi Mtendaji kupitia anuani ifuatayo: -

MKURUGENZI MTENDAJI,

HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO,

328 BARABARA YA SABASABA,

S.L.P 52,

25782 MKUU – ROMBO.

xi. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 24/6/2026 saa 9:30 Alasiri.

Maombi Yatatumwa kwa Njia ya Posta au Kwa Kupeleka Barua kwa Mkono

DOWNLOAD