Umuhimu wa Joto kwa Vifaranga
Usimamizi wa joto ni moja ya mambo muhimu zaidi katika ufugaji wa vifaranga vya kuku. Wafugaji wengi hupoteza vifaranga ndani ya wiki za mwanzo si kwa sababu ya magonjwa, bali kutokana na joto lisilofaa. Vifaranga wadogo hawawezi kudhibiti joto la mwili wao vizuri, hivyo hutegemea mazingira ya banda kupata joto sahihi.
Umuhimu wa Joto kwa Vifaranga
Joto sahihi husaidia:
- Ukuaji wa haraka
- Kinga nzuri ya mwili
- Matumizi mazuri ya chakula
- Kupunguza vifo vya vifaranga
- Kuzuia msongamano na kudhoofika
Ukikosea joto kwenye siku 14 za mwanzo, hata chakula bora hakiwezi kurekebisha madhara yote yaliyotokea.
Viwango vya Joto Vinavyopendekezwa kwa Vifaranga
| Umri wa Kifaranga | Joto Linalotakiwa |
|---|---|
| Wiki ya 1 | 32–35°C |
| Wiki ya 2 | 29–32°C |
| Wiki ya 3 | 26–29°C |
| Wiki ya 4 | 23–26°C |
Baada ya wiki ya 4, vifaranga wengi huanza kuhimili mazingira ya kawaida kutegemea hali ya hewa.
Dalili za Joto Lisilofaa kwa Vifaranga
Vifaranga Wakipata Baridi
Dalili
- Kukusanyika pamoja chini ya taa
- Kelele nyingi
- Kula chakula kidogo
- Kukua polepole
Madhara
- Vifo kutokana na kukanyagwa
- Kushuka kwa kinga
- Kuongezeka kwa magonjwa
Jinsi ya Kurekebisha
- Ongeza joto kwa kusogeza taa karibu na vifaranga
- Ziba sehemu zinazoingiza upepo mkali bandani
- Hakikisha bedding ni kavu muda wote
- Tumia thermometer kufuatilia kiwango cha joto
- Epuka msongamano mkubwa wa vifaranga
Vifaranga Wakipata Joto Kupita Kiasi
Dalili
- Kutawanyika mbali na chanzo cha joto
- Kupumua kwa haraka
- Kufungua midomo mara kwa mara
- Kunywa maji mengi kuliko kawaida
Madhara
- Kupungua kwa appetite
- Kukua kwa shida
- Upungufu wa maji mwilini
Jinsi ya Kurekebisha
- Punguza joto kwa kuinua taa juu zaidi
- Hakikisha banda lina hewa ya kutosha
- Weka maji safi ya kutosha muda wote
- Epuka taa kali sana ndani ya banda
Hitimisho
Joto sahihi ni msingi mkubwa wa mafanikio katika ufugaji wa vifaranga. Wafugaji wengi hupata hasara kubwa kutokana na kupuuza usimamizi wa joto kwenye wiki za mwanzo. Ukizingatia viwango sahihi vya joto, usafi wa banda, maji safi na lishe bora, utaongeza ukuaji wa vifaranga na kupunguza vifo kwa kiwango kikubwa.
Barikiwa sana.
Post a Comment