Jinsi ya Kudhibiti Mafua ya Kuku Kwenye Shamba la Kisasa
Jinsi ya Kudhibiti Mafua ya Kuku Kwenye Shamba la Kisasa
Ili kuyadhibiti mafua ya kuku, zingatia yafuatayo vizuri. Ni lazima kuwe na mfumo mzima wa usimamizi wa afya ya kuku kuanzia banda, chanjo, usafi, hewa ya banda, maji, chakula pamoja na biosecurity.
Chanzo Kikubwa cha Mafua Kwenye Mashamba
Mafua mengi ya kuku husababishwa na:
- CRD / Mycoplasma
- Infectious Coryza
- Newcastle Disease (ND)
- Infectious Bronchitis (IB)
Mara nyingi magonjwa haya huingia kutokana na:
- Msongamano mkubwa wa kuku
- Banda lisilo na hewa ya kutosha
- Vumbi na amonia nyingi
- Ile harufu inayopanda ukiingia bandani na kuumiza macho
- Kuchanganya kuku wa umri tofauti
- Wageni kuingia hovyo bandani
- Rafiki yako akija unampeleka bandani au kuingiza watu ovyo ni hatari
- Kutokufuata ratiba ya chanjo
- Stress kwa kuku
- Kutokukunga au kusafisha mavumbi ya maranda
Mfumo wa Kudhibiti Mafua Shambani
Biosecurity
Ulinzi wa shamba ni muhimu kuliko vyote. Wazungu wamefanikiwa sana hapa boss. Hii ndiyo nguzo kubwa kuliko hata dawa.
Mambo Muhimu ya Kuzingatia
- Watu wasiingie hovyo bandani
- Tumia viatu maalum vya banda
- Weka footbath yenye disinfectant kila mlango wa banda
- Osha vifaa vya kulishia na kunyweshea kila siku
- Ondoa kuku wagonjwa mara moja
- Kuku waliokufa wazikwe au wachomwe haraka
Footbath nzuri:
- Virkon
Disinfectant ibadilishwe mara kwa mara ili ibaki na nguvu.
Usimamizi wa Banda
Banda lina mchango mkubwa sana kwenye magonjwa ya mfumo wa hewa.
Banda bora linapaswa:
- Kuwa na hewa ya kutosha
- Kusiwe na unyevu mwingi
- Kutokuwa na vumbi nyingi
- Kusiwe na harufu kali ya amonia
Madhara ya Amonia
Amonia huharibu mfumo wa upumuaji wa kuku na kufanya mafua yawe sugu hata baada ya dawa.
Hatua Muhimu
- Badili litter mara kwa mara
- Usimwage maji kwenye bedding
- Epuka overcrowding
- Hakikisha ventilation nzuri hasa usiku
Mfumo wa Chanjo kwa Kuku
Chanjo muhimu ni pamoja na:
- Newcastle Disease
- Infectious Bronchitis
- Gumboro
- Fowl Pox
Chanjo hizi husaidia kuzuia respiratory diseases, kuongeza immunity na kupunguza maambukizi mbalimbali ya kuku.
Matumizi Sahihi ya Dawa kwa Mafua ya Kuku
Makosa makubwa yanayofanywa na wafugaji wengi ni:
- Kuchanganya antibiotics nyingi
- Kubadilisha dawa kila siku
- Kutotumia dozi sahihi
- Kutomaliza treatment course
Mfumo Sahihi wa Tiba Kwenye Respiratory Outbreak
Tumia antibiotic moja tu:
- Tylosin
- Enrofloxacin
- Oxytetracycline
Tumia kwa siku 3 hadi 5 mfululizo.
Supportive Treatment
- Vitamins
- Electrolytes
- Probiotics
Umuhimu wa Probiotics kwa Kuku
Baada ya kutumia antibiotics:
- Mfumo wa digestion huharibika
- Kinga hushuka
Probiotics husaidia:
- Kurudisha bacteria wazuri tumboni
- Kuongeza appetite
- Kuimarisha immunity
Mfumo wa “All In All Out”
Kwa mashamba makubwa ni muhimu sana.
Maana yake:
- Kuku wanaingia pamoja
- Wanatoka pamoja
- Banda linaoshwa na kupumzishwa kabla ya batch nyingine
Faida Zake
- Kupunguza disease carryover
- Kupunguza mafua ya kurudia
Dalili Zinazoonyesha Mafua Yamekuwa Makubwa
Ukiona:
- Kukoroma sana usiku
- Kamasi nyingi
- Kuku kupumua kwa mdomo
- Uso kuvimba
- Kula kupungua
- Vifo kuanza
Usisubiri sana kubadilika yenyewe. Anza management mapema.
Hitimisho
Kwa sasa mafua ya kuku ni moja ya changamoto kubwa kwenye poultry industry. Suluhisho si kutumia dawa nyingi bali ni kuwa na mfumo mzuri wa:
- Biosecurity
- Chanjo
- Usimamizi wa banda
- Matumizi sahihi ya dawa
Ukizingatia haya utaokoa gharama zako na kupunguza magonjwa mengine, si mafua tu.
Post a Comment