Majina ya Walioitwa Kazini 04-07-2026
Majina ya Walioitwa Kazini 04-07-2026
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) imetangaza rasmi matokeo ya usaili wa ajira kwa waombaji waliofanya usaili katika kipindi kilichobainishwa. Tangazo hili linajumuisha majina ya waombaji waliofanikiwa kupata nafasi za kazi pamoja na baadhi ya waombaji waliokuwa kwenye kanzidata (Database) ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.
Waombaji wote waliochaguliwa wanapaswa kuingia kwenye Ajira Portal, sehemu ya "My Applications", ili kupakua barua zao za kupangiwa kazi na kuzitumia wakati wa kuripoti kwa mwajiri.
Wakati wa kuripoti, waombaji wanatakiwa kufika ndani ya muda uliowekwa kwenye barua ya ajira wakiwa na vyeti halisi vya elimu na taaluma kwa ajili ya uhakiki kabla ya kukamilisha taratibu za kuajiriwa.
Kwa waombaji ambao majina yao hayajaonekana kwenye tangazo hili, wanashauriwa kuendelea kufuatilia matangazo mapya ya ajira na kuomba nafasi zitakapotangazwa tena.