Walimu wa Kujitolea wa Somo la Elimu ya Biashara Waliochaguliwa 2026
Tamisemi Majina ya Walioitwa Kazini Somo la Business Studies 2026
Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI kwa kushirikiana na Educate! Tanzania imetangaza majina ya walimu wa kujitolea wa somo la Elimu ya Biashara waliochaguliwa kufundisha kwa mkataba katika shule za sekondari zenye uhitaji mkubwa. Walimu wote waliochaguliwa wanapaswa kuripoti katika Halmashauri walizopangiwa kuanzia 24 Julai hadi 6 Agosti 2026 kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kuanza kazi. Orodha ya majina ya waliochaguliwa inapatikana kupitia mfumo wa Ajira TAMISEMI na tovuti rasmi ya TAMISEMI.