Sifa za Kujiunga Mafunzo ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi 2026/2027

June 10, 2026

Sifa za Kujiunga Mafunzo ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi 2026/2027

Sifa za Kujiunga Mafunzo ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi 2026/2027

Waombaji wanaotaka kujiunga na Mafunzo ya Ualimu ngazi ya Stashahada wanapaswa kukidhi vigezo vya kitaaluma vilivyowekwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Sifa za kujiunga zinatofautiana kulingana na aina ya programu ya mafunzo inayotolewa, kama ilivyoainishwa hapa chini.

SIFA ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU

a) Sifa za kujiunga na Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi (Miaka 02)

(i) Wahitimu wa Kidato cha Sita wenye ufaulu wa Daraja la I–III kwa kiwango cha “Principal Pass” mbili (02); na

(ii) Walimu waliohitimu Mafunzo ya Ualimu ngazi ya Astashahada (Cheti) ya Ualimu wa Elimu ya Awali au Msingi. Aidha, waombaji watakaochaguliwa watapangwa kwenye mikondo kulingana na ufaulu wao katika Mtihani wa Taifa wa Ualimu ngazi ya Astashahada.

b) Sifa za kujiunga na Stashahada Maalumu ya Ualimu Elimu ya Msingi (Miaka 03)

Wahitimu wa Kidato cha Nne wenye ufaulu wa Daraja la I–III kwa kiwango cha alama “C” au zaidi katika masomo matatu, ambapo mawili kati ya hayo yawe ni:

  • Basic Mathematics
  • Biology
  • Chemistry
  • Physics
  • Information and Computer Studies
  • Computer Science

c) Sifa za kujiunga na Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi kwa njia ya Masafa (Miaka 03–04)

Walimu waliohitimu Mafunzo ya Ualimu ngazi ya Astashahada (Cheti) ya Ualimu wa Elimu ya Awali au Msingi.

Vyuo vya Ualimu vyenye nia ya kuendesha Mafunzo ya Ualimu kwa njia ya Masafa vinapaswa kuzingatia masharti ya Mwongozo wa Utoaji wa Mafunzo ya Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Awali na Msingi kwa njia ya Masafa (Februari 2026) uliotolewa na Kamishna wa Elimu. 

UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI NA KUPOKEA MAJIBU

Utaratibu wa kutuma maombi na kupokea majibu kwa waombaji wa Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi na Stashahada Maalumu ya Ualimu Elimu ya Msingi utakuwa kama ifuatavyo:

(i) Wahitimu wa Kidato cha Nne, Kidato cha Sita na Walimu waliohitimu Astashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi wenye sifa zilizobainishwa katika tangazo hili wanaruhusiwa kutuma maombi.

(ii) Waombaji wa Mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali wanatakiwa kujisajili na kutuma maombi kielektroniki kupitia mfumo wa udahili wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (https://tcm.moe.go.tz/).

(iii) Mwombaji wa Mafunzo ya Ualimu ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi (Miaka 02) atachagua michepuo mitatu (03), akianza na ule anaoupenda zaidi.

(iv) Mwombaji wa Mafunzo ya Ualimu ya Stashahada Maalumu ya Ualimu Elimu ya Msingi (Miaka 03) atachagua tahasusi tatu (03), akianza na anayoipenda zaidi.

(v) Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali yatatolewa kupitia akaunti aliyotumia mwombaji kuwasilisha maombi (kuanzia tarehe 15/07/2026) pamoja na katika vyuo walivyopangiwa.

(vi) Waombaji wa Mafunzo ya Ualimu katika Vyuo visivyo vya Serikali watatuma maombi moja kwa moja katika vyuo husika. Aidha, majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na mafunzo hayo yatatolewa na vyuo walivyochaguliwa.

(vii) Fomu za maelekezo ya kujiunga na Mafunzo ya Ualimu zitatolewa kupitia tovuti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (www.moe.go.tz) na kupitia chuo atakachopangiwa mwombaji kwa kutumia anuani yake. Waombaji wote wanashauriwa kuandika anuani kamili, barua pepe na namba ya simu inayopatikana kwa mawasiliano.

(viii) Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 10 Julai 2026. 

PAKUA PDF HAPA